By Jean Damascène Hakuzimana

Novemba 7 Alpha Conde mwenye umri wa miaka 82 alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Guinea ambao ulimpa kipindi cha tatu chenye utata katika ofisi ya Guinea . Ivory Coast, nchi jirani ya kusini ya Guinea pia hivi karibuni walimchagua tena rais wao Alassane Ouattara mwenye umri wa miaka 78 kwa muhula wa tatu. Waunaume hawa wote wawili walijiunga na kilabu kinachokuwa zaidi na zaidi cha marais wa Afrika ambao wametafuta nyongeza ofisini licha ya katiba kutoruhusu zaidi ya mihula miwili

Wanachama wa kilabu hiki cha marais wamebuni njia za kuzirekebisha katiba za nchi zao na kuondoa vikwazo vilivyowafanya wasigombee mihula ya nyongeza ofisini. Wagombea hutumia mbinu tofauti tofauti lakini matokeo ni yaleyale . Kwa mfano Alpha Conde alianza “ kampeni ya kutimiza alichoanza katika kipindi cha awali”. Alassane ouattara amedhihirisha kugombea kwake kama kutimiza “ hamu na matakwa ya taifa” baada ya kifo cha ghafla cha mgombea ambaye alikuwa akimtayarisha kwa ofisi. Alikuwa amedhamiria kutoona mamlaka yakienda kwa upinzani wa waziri mkuu wa zamani Pascal AffiN’Guessan Marais wengine wamekuwa madarakani hata zaidi ya vipindi vitatu. Rais Museveni wa Uganda amefanya kampeni ya kuondoa kabisa mipaka ya umri katika katiba hivyo kwamba anaweza kugombea tena baada ya miaka 34 ofisini- kulingana na katiba ya Uganda rais hawezi kuwa mdogo chini ya miaka 35 au zaidi ya miaka 75. Hapo awali alifutilia mbali mipaka ya muda ya awamu ya urais. Museveni ni miongoni mwa watano waliohudumu kwa muda mrefu zaidi ya marais wa Afrika pamoja na Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Guinea ya Ikweta .ambaye amekuwa madarakani tangu 1979. Marais wengine ambao wameshikilia madaraka kwa miongo kadhaa ni pamoja na Paul Biya wa Kamerun –rais tangu 1982 : Denis Sassou Nguesso wa Kongo Brazza-Ville –ofisini kwa zaidi ya miaka 36:
Idriss Debby wa Chad. Rais kwa miaka 29.

Mihula ya ziada mara nyingi husababisha vurugu na wakati mwingine husababisha kifungo cha gerezani na vifo.Kwa mfano hiyo ndiyo hatima ya Pascal N’Guessan ambaye alitiwa mbaroni Jumamosi Novemba 7 chini ya mashtaka ya ugaidi baada ya majeshi ya serikali kupigana na wa upinzani. Mapigano yalisababisha vifo vya zaidi ya raia 40 wa Ivory Coast. Matumaini ya mabadiliko mara nyingi hupotea kadri rais anapong’ang’ania ofisi. Hivyo ndivyo anavyoimarisha nguvu zake zaidi na kuikandamiza upinzani zaidi.

Julai 28, 2015, akihutubia Umoja wa Afrika. Rais Obama alisema, “wakati kiongozi hujaribu kubadilisha sheria katikati ya mchezo ili kukaa ofisin ni hatari na huleta ugomvi na mara nyingi ni hatua ya kwanza tu kwenye njia hatari.” Muungano wa Afrika umekuwa kimya kuhusu mabadiliko ya kura za urais .

Mfano wa kushikamana na nguvu na ukandamizaji wa watu umesababisha kuondoka Waafrika wengi, ambao wamekimbia mateso katika nchi zao ,na kuhamia nchi na majimbo mengine [kama Maine], kuendeleza ukuaji wa Waafrika waishio nje ya bara lao.. Katika nakala katika Daily Maverick , Mmusi Maimane .wakati mmoja kiongozi wa muungano wa kidemokrasia wa upinzani wa Afrika kusini alisema “tumeona kila wakati wakombozi wanaingia madarakani huku wakiahidi kuleta mabadiliko huku nia yao ikiwa ni ufisadi . Tumeona mfumo wa marais wanaojiita `Big Man’ kujilimbikizia mali kwa kiwango kisichowezekana kwa raia wa kawaida ‘ Maimane alionya kuwa ni wakati wa kupitishwa umri wa makamo. ‘‘Afrika inahitaji vijana na uongozi wenye uwezo ,bila uhusiano wowote na harakati za ukombozi wa zamani.