Na Bright Musuamba – Mratibu wa program, ProsperityME

Nilipokuwa nikikuwa, siku zote nilijisikia ilinibidi kudhani hali ya wazazi wangu kila mara ilitubidi kuzungumza juu ya pesa.Ninaporudisha macho nyuma, ninadhani walikuwa wazi kama walivyofikiria wanaweza kuwa lakini, nilijua wakati tulihanagika na wakati gani tulikuwa bila shida. Mara nyingine ilinibidi kudhani(bila uhakika) wakati ilikuwa sawa kwa kuomba pesa za mfukoni

Kwa maoni yangu, ni muhimu kwa jamaa kuongea juu ya usalama wa kifedha .Pesa ni sehemu ya mazungumzo lakini sio mazungumzo yote. Kuzungumzia pamoja kuhusu mipango na malengo ya kifedha inaweza kukuza heshima na uaminifu.Inaweza kuhamasisha kila mmoja kutumika pamoja na wengine kufanya ndoto zigeuke ukweli

Nadhani kuna mambo matatu jamaa na vijana wangalipaswa kujizoeza kuongea pamoja kwa kuanza kujenga usalama wa kifedha:

1.Tunahitaji kufanya kazi ili kuondoa unyanyapaa nyuma ya mazungumzo ya kifedha kati ya wazazi na watoto. Wazi, kuongelesha watoto wenu kuhusu pesa haimaanishi kwamba mnawabebesha mizigo ya watu wakubwa! Inamaanisha kuwa mnawafikiria/ mnawaheshimu na kuwajumuisha kwenye mada zinazojumuisha na kuathiri jamaa nzima.

2.Watoto,muwe wangalifu, wenye hamu ya kujifunza, na kuuliza maswali. Wakati mwingine sisi vijana huwa na ujinga na hatujali sana kujihusisha na maswali ambao tuadhani ni “ya watu wazima tu”.Hapana!Kuyazungumzia maswali tunayoyaita “magumu” inaweza kutusaidia mwishowe. Wazi wangu wamenifundisha ujuzi muhimu sana ambao ninaendelea kutumia hadi leo. Wamenifundisha jinsi ya kufanya bajeti, kufanya akiba na thamani ya pesa iliopatikana kwa bidii. Ustadi huu hutupa hatua ya kuruka, haswa katika jamii ya leo ya mabepari

3. Wazazi, jitahidi kujifunza na kufundisha watoto wenu ujuzi wa kifedha! Kama wahamiaji, tunakuja nchini Marekani na tunapaswa kuanzilia kila kitu na kujifunza vitu vingi kutoka mwanzo. Inatubidi tujifunze mfumo wa mikopo, kujenga historia ya mkopo na kupata msingi mzuri wa kifedha ili tusije tukaangukie katika deni mbaya na maamuzi ya kifedha. Nilipokea mara nyingi onyo maarafu kwamba pesa haikui kwenye miti hivyo nikajua tangu umri wangu mdogo umuhimu wa pesa.Uhuru wa kifedha ndio lengo langu kuu la maisha lakini kwa sasa nitaunda dhamana na usalama wa kifedha

Hivi karibuni nilichukua jaribio ili kujua utu wangu wakifedha: niliitwa “mhifadhi” msemo ambao nilidhani ulikuwa sahihi sana. Asante kwa ushawishi wa wazazi wangu. Mimi ni mtu makini sana kwa kuwekeza pesa zangu, kupanga kwa siku zijazo, na kuwa na usalama wa kifedha. Kwa sababu ya tabia hizi, jamma yangu wamejifunza kunitegemea ijapokuwa mimi ni mzaliwa wa mwisho.Wanajuwa wanaweza kunitegemea kwa kushikilia pesa kiasi fulani, kuwekeza pesa zao, ama ikiwa wahitaji kuongea kuhusa pesa. Ninajivunia na nimefurahi kuweza kusaidia jamaa yangu kwa njia hiyo, haswa kama mhamiaji na kijana. Kila maarifa ya kifedha ninayopata mimi hushirikisha jamaa yangu ili tukuwa na kubadilisha maisha pamoja

Tuna uwezo mwingi ndani na tunaweza kufikia na kutenda mambo mengi ikiwa tunasukumia kujifunza na kushirikisha wengine habari tunazozipata. Mambo ya fedha hayapaswi kututisha wala kutuogopesha lakini badala yake, fedha zinapaswa kutuhamasisha na kutushinikiza kusonga mbele na kutuhimiza kuwa na ndoto kubwa. Chochote kinawezekana ikiwa hatujiwekei kikomo wenyewe!

Kuhusu mwandishi: Bright ni mzaliwa wa Kongo ya Kidemokrasia ambaye alihamia mjini Lewistonmiaka mitano iliyopita. Bright huzungumza lugha tatu na ana shauku ya kuwawezesha, waelimisha na kuwainua watu binafsi kupitia kazi nayoyifanya pa ProsperityME. Bright anahisi kuwa anafafanuliwa vizuri na nukuu kutoka kwa Maya Angelou ambayo inasoma, “Dhamira yangu maishani sio tu kuishi lakini kustawi, na kufanya hivyo kwa shauku Fulani, ucheshi Fulani, na mtindo Fulani”

Ukitaka kuifunza zaidi kuhusu program zetu zuwezeshaji wa kifedha, tafadhali fikia Bright kupitia anwani ya elektroniki yake [email protected]