Kwa yeyote atakaye kuomba mkopo wa biashara, ajuwe kwamba kulingana na jinsi biashara imeandaliwa, kuomba mkopo wa biashara inaweza kuwa mchakato mgumu ama rahisi, kulingana na mmiliki wa biashara amejiandaaje. Sababu ni kwamba pesa ambazo programu zingine za mkopo zinao ni chache, na zinaweza kuisha haraka, mmiliki wa biashara anaweza kukusanya makaratasi yanayohitajika kuomba, ndivyo anavyoweza kupata jibu haraka ikiwa ataweza kupata mkopo ama hatapata.

La pili ni hili: biashara ikitayarishwa , mkopeshaji atakuwa na picha halali ya fedha za biashara mapema katika mchakato, na hii inaweza kufupisha mchakato wa maombi.Hapa chini tunazo nyaraka za kawaida ambazo mkopeshaji anaweza kuhitaji na ambazo anapaswa kuwa nazo kwa mkono  kila wakati .

 

Habari kutoka  benki

Uimara na historia ya biashara vinaweza kuonekana kupitia mkusanyiko wa habari za  biashara kutoka kwenye benki . Habari hizi pia zinaonyesha jinsi gani pesa zilivyotumiwa, na hizo habari zinaweza kuwa muhimu baadaye kwa mipango fulani ya mkopo

 

Kurudishwa kwa ushuru

Juwa kwamba yeyote atakaye kurudishiwa ushuru, kwa kawaida, miaka mitatu ya malipo ya ushuru kwa serikali ya shirikisho yatakikana.Lakini, ikiwa  bado biashara hii ingali inaanza haijapita muda mrefu, marejesho machache yatahitajika.

 

                                                   

 

Habari za kibinafsi za kifedha

 Habari kuhusu mali na madeni ya yule ambaye anahitaji mkopo wa biashara zapatikana kwa ufupi  katika nyaraka hii. Hapa mali yamaanisha  chochote ambacho mwombaji wa mkopo anachomiliki, kwa mfano gari, au ardhi. Madeni ni gharama ama   mikopo amabayo mwombaji anaweza kudaiwa pesa, kwa mfano rehani ya nyumba. Wakati wa taarifa ya binafsi ya kifedha ya mwombaji, mapato ya mwombaji yanazingatiwa.Mali, deni, na wavu wa mwombaji vyote vinazingatiwa katika mchakato wa idhini ya mkopo.

Habari kuhusu  faida na hasara

Habari hizi ni  kuhusu mapato na gharama za kampuni ya kufanya biashara. Taarifa ya faida na upotezaji inaonyesha waziwazi  ikiwa biashara inaweza kutoa faida ama kwa kuongeza mapato na/au kupunguza gharama

Karatasi ya mizani

Karatasi ya usawa inaonyesha jinsi fedha za kampuni zinafanya kwa mfano ukichukuwa tarehe fulani. Inapana habari kuhusu mali zote, deni na usawa wa wenhye hisa. Usawa wa mwenye hisa ni kiwango cha pesa amabacho wamiliki wa kampuni wamewekeza katika biashara hiyo

Mpango wa biashara

Mpango wa biashara unatambua mwenendo, na unaandika jinsi na kwa nini biashara itafanikiwa. Ni njia ya kuwasiliana na mtu yeyote ambaye anaisoma ikiwa na kusudi la kuwaelewesha kwa nini wanapaswa kuamini biashara hii na kuwekeza ndani yake

Leseni za biashara

Leseni za biashara zina lengo la kuonyesha mkopeshaji jinsi biashara imeundwa.Kwa mfano, biashara inaweza kuwa LLC, S-Corp, umiliki wa pekee, ama shirika lisilo la faida.Hizi ni njia ambazo zinazowezesha serikali kutambua biashara. Kwa kila moja, kuna sheria tofauti  Wahasibu ama wawekaji hesabu ni wataalam wa kuweka  hati hizi pamoja ili kusaidia kampuni kuomba mikopo ya biashara. Kwa vinginevyo, kuna vifurushi vya program na tovuti ambazo wafanyabiashara wanaweza kulipa ili kutoa hati muhimu za mkopo. Mara nyingi hupatikana mashirika ya jamii ambayo husaidia wafanyabiashara wadogo wenye kuhitaji mkopo wa biashara.

 

Unapofika wakati wa kuomba, hakikisha kuuliza orodha ya kuangalia hati zote ambazo mkopeshaji au program inahitaji kushugulikia mkopo.. 

Usisahau kwamba vitu vya ziada vinaweza kuombwa wakati wa mchakato wa mkopo. Uliza kuhusu tarehe zozote za mwisho ambazo mkopeshaji anazo  kwa kukabidhiwa makaratasi, na kujitolea kwa tarehe hiyo ya mwisho. Ikiwa lazima ukose tarehe ya mwisho, tarajia hiyo mapema, na zungumza na mkopeshaji. Weka makaratasi yote yamepangwa na salama -hizi ni hati za kibinafsi ambazo zinapaswa kushirikiwa tu na vyanzo vya kuaminika

Kwa kujitayarisha mapema, wamiliki wa biashara wanaweza kufurahiya uzoefu mzuri wakati wa kuomba mkopo wa biashara. Habari sio kwamba tu inafichua picha kamili ya fedha za kampuni kwa mkopeshaji, lakini biashara itapata kuelewa wazi afya zao kifedha pia.