“ Umwami mwiza akamari rubanda rwose ,abakene nabakire”
“Kiongozi maalum husaidia kila mwanamemba wa taifa lake, akiwa tajiri ao mkosefu”
Miongoni mwa walioalikwa kwa kuhudhuria tarehe 2 Januari kwenye uzinduzi kihistoria kwenye Kituo cha Urahia cha Augusta kupewa mtawala mwanamke wa kwanza katika historia jimbo la Maine walikuwamo viongozi wengi wa jumuiya za wahamiaji. Waliozungumza na Amjambo Africa! baada ya sherehe hizo wamesema kwamba hii ni mara yao ya kwanza kualikwa kwenye tukio la kisiasa la ngazi ya umuhimu kama huu humu Maine. Mnamo tarehe 4 Januari, wahamiaji wengi pia walialikwa na Gavana Janet Mills kwenye sherehe hilo. Walionyesha kuridhika sana kwa kukaribishwa katika matukio hayo yote na kugawana msamaha wao kwamba miaka nane ya utawala wa Gavana Paul LePage sasa imeisha, na kwamba zama mpya, ya umoja zaidi imeanza Maine.
Watoto watatu wazaliwa wa Afrika walishirikishwa kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi. Watoto hao walikuwa ni Alain Igiraneza, mwanafunzi katika Shule ya sekondari ya Casco Bay, kutoka Burundi, ndiye aliimba wimbo wa kitaifa; Shy Paca na Natalia Mbadu, kutoka Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mtiririko huo, wanafunzi wote wawili hushiriki shule la Reiche, ambao waliimba “Binti kwene moto” “Girl on fire” iliyotungwa na Alicia Keys. Kuimba kwa watoto hao kulikuwa kwa moyo mzuri na wenye nguvu hata kuleta umati wa watu kusimama. Batimbo United, kikundi cha wapiga ngoma na wachezaji wa Burundi kutoka Portland, walifanya maonyesho kwenye uzinduzi huo.
Uchaguzi wa Gavana Mills unaonyesha wazi jinsi mwendo wa kisiasa ulivyo tofauti hapa Marekani tofauti na kile Waafrika wengi walioishi nyumbani. Katika nchi za Kiafrika, kupeana madaraka baada ya uchaguzi mara nyingi hufunikwa na wingu la matetezi ya kuibiwa kwa kura. Vurugu na vita na vita wya kiraia – au uvumi wa hayo – husababisha watu kuwa na hofu baada ya uchaguzi, badala ya kusherehekea. Mara nyingi, watu hukaa ndani ya nyumba siku baada ya uchaguzi, kwa sababu ya hofu ya vurugu. Wakaaji wapya wa Maine waliozaliwana kukua chini ya uongozi, au viongozi wenye mamlaka, wanajifunza mengi kutokana na uhamisho wa amani wa madaraka hapa Maine. Wanatambua kwamba juma la muzinduo huku Maine umekuwa furaha na wa amani, na walishangaa kuona jinsi demokrasia iliyopo kazini hapa nchini Marekani.
Janet Mills’ huthamini sana umoja na ushirika ulio onekana wenye mwanga mkuu kupitia wiki lote la matukio ya uzinduzi. Ameonyesha nia yake ya kubadilisha alama iliyo kwa mlango wa kuingia Maine kutoka New Hampshire na msemo mmoja, Karibu nyumbani, inayo sikilika kupendwa sana na wale wanaokuja kujenga maisha yao mapya humu Maine.
- Alain Michel Igiraneza sings the National Anthem
- Alain Michel Igiraneza sings the National Anthem







