Ni watu wengi ambao wanahitaji kutuma pesa nyumbani kusaidia wapendwa wao . Kwa bahati mbaya, mara moja na moja pesa hii iliyopatikana kwa jasho haifikii yule anayestahiki. Watapeli hupenda uhamisho huu wa pesa kwa sababu unawapa njia ya haraka na rahisi ya kupata pesa. Soma ili upate vidokezo fulani vya jinsi ya kuhakikisha pesa zako ziko salama na zitamfikia yule ambaye anapaswa zipewa huko nyumbani.

Kuna vidokezo vya jumla hapa kuhusu kuweka pesa zako salama:
• Usitoe hata mara moja kuhusu maelezo ya kibinafsi kama nambari yako ya usalama wa kijamii, nambari za akaunti, au habari ya benki kwa watu ambao hujawaomba au mtu yeyote kupitia maandish mafuti ya simui au barua pepe.
• Hakikisha vifaa vya elektroniki nivya kisasa na viko salama.
• Hakikisha muunganisho wa mtandao unaotumia uko salama.
• Usitumie waya kwa kumuwekea pesa mtu usiyemjua.
• Angalia taarifa za kifedha mara kwa mara ili uweze kupata miamala yenye tuhuma.
• Benki na vyama vya mikopo huuliza maswali na nia ya kumlinda mtumaji wa pesa, kwa hivyo ni yenye usalama zaidi kujibu kwa uaminifu maswali yoyote unayoulizwa.

 


Hapa kuna vidokezo kuhusu chaguzi tofauti za kutuma pesa:
Uhamisho wa waya katika taasisi yako ya kifedha: Unaweza kuhamisha ama kutuma pesa zako kwa uhamisho wa waya ukisaidiwa na vyama vya mikopo na benki pia , vilevile zasaidia kwa matumizi ya mtu-kwa-mtu, na zaidi. Uhamisho wa benki na umoja wa mikopo ni salama sana kwa sababu fedha zinahamishwa kutoka benki moja kwenda nyingine, na safu za usalama zilizojengwa. Watumaji wanahitaji kuthibitisha ni nambari gani ya kutumia na wakati mwingine benki zina nambari tofauti ya kuhamisha, kama vile nambari ya SWIFT. SWIFT inasimama kwa Jumuiya ya Mawasiliano ya Fedha Duniani ya Interbank, ambayo inamaanisha nambari ni kama nambari ya upitishaji ya kimataifa.

Kampuni za kuhamisha pesa kwa njia ya waya: Watumiaji hubadilishana sarafu na pia kutuma pesa zao nyumbani na kimataifa wakisaidiwa na kampuni hizi (kama Western Union ama MoneyGram). Huduma hizi nyingi ni za kuaminika sana kufuatana na sera za kuzuia udanganyifu na zina sehemu kwenye wavuti zao zilizojitolea kuelimisha wateja wao kuwaweka salama.
.
Programu za simu: Kuna programu fulani kama PayPal, Google Pay, na Venmo ambazo ni rahisi kuchukua kwenye mtandao na zinaweza kutumika kutuma pesa kwa marafiki. Ni rahisi na ya haraka, na kawaida huwa bure, lakini vilevile ni rahisi kufanya makosa na kutuma pesa kwa mtu asiyefaa. Kuna uwezekano mdogo wa mizozo ikiwa kuna kosa au shughuli ya ulaghai

Akaunti ya benki ya uhamishaji wa pesa: Kuna watu ambao hufungua akaunti ya pili ya benki, tofauti na akaunti yao ya kawaida ya benki, kwa pesa tu ya kutuma nyumbani. Mwanzoni, hii inasababisha kazi ya ziada, lakini mara tu mfumo unapowekwa tayari, inaweka pesa kwenye akaunti yako ya kawaida salama. Udanganyifu ukitukia, matapeli hawatapata pesa zako zote.