Na Julia Brown
Immigrant Legal Advocacy Project (ILAP) ndiyo shirika la kipekeelenye kukubalika kisheria nchini Maine linaloshughulika na maswala ya wahamiaji. Iangalie tovuti yetu kupata habari zaidi: https://www.ilapmaine.org .
Utawala na Utendakazi wa Biden. Rais Joe Biden aliichukua ofisi mnamo Januari 20 na kwa sasa ameleta mageuzi ya haraka kwa wahamiaji ikiwemo: Kuondoa marufuku ya Uislamu na usafiri wa waafrika. Rais Biden aliukomesha ubaguzi wa uislamu na wa usafiri kwa kubagua au kupendelea rangi fulani. Kuhifadhi na kuipa nguvu Deferred Action for Childhood Arivals (DACA). Rais Biden aliamrisha katibu wa Department of Homeland Security (DHS) achukue hatua zote ambazo ni sawa na zinaambatana na sheria husika, kuhifadhi na kuipa nguvu DACA. Kusimamisha ujenzi wa ukuta wa mpaka, kusimamisha Migrant Protection Protocols (wabaki Mexico ). DHS imetupilia mbali Migrant Protection Protocols (MPP), ambayo iliwalazimu wahamiaji wa mpaka wa kusini kusubiri Mexico kwa kikao cha mahakama huko U.S. DHS vilevile imetangaza utaratibu wa kuzisaidia familia ambazo kwa sasa bado zimekwama katika programu hii. Kuachwa kwa muda uhamisho fulani na ubadilishe vipaumbele vya utekelezaji wa uhamiaji au DHS ilitoa kumbukumbu na kuelezea mabadiliko kadha muhimu ya sera. Pamoja na kusitisha uhamisho fulani kwa siku 100 na vipaumbele vipya vya utekelezaji wa wahamiaji. Kusitishwa kwa uhamisho kumesimamishwa kwa muda wa sheria ya shirikisho linaloitwa kuweka na kupanua ulinzi wa ukombozi kwa rais wake Biden. Rais Biden ameongoza “ kuondoka kwa utekelezaji” (DED) kwa waliberia hadi tarehe 30 Juni 2022. Rejesha hesabu kamili ya sense. Rais Biden alibadilisha jaribio la zamani la Trump lisilo halali la kuwatenga wahamiaji wasio na hatia kutoka katika hesabu ya sensa.Kuunda kikosi cha kazi cha kuunganisha familia zilizotengwa.Rais Biden alitoa agizo la utendaji la kuunda kikosi cha kazi cha kutambua watoto wote waliotenganishwa na sera za kutokuwa na uvumilivu wa Rais wa zamani Trump na kuwaunganisha tena na familia zao.Kushughulikia mgogoro wa hifadhi wa kusini.Rais Biden alitoa amri ya mtendaji kushughulikia shida zinazowakabili wanaotafuta hifadhi katika mpaka wa kusini.Mipango mingine ya kusaidia misaada na mipango ya kupambana na ufisadi Amerika ya kati, na kuanzisha tena mpango wa watoto na vijana kutoka Amerika ya kati (CAM).Agizo linaamuru katibu wa DHS atumie sheria na sera kadhaa za kupambana na hifadhi na kukagua kuondolewa haraka mipango ambayo ni michakato ya kwanza ya kuhamishwa bila kusikilizwa.Kuboresha mfumo wa uhamiaji .Rais Biden pia alitoa amri ya mtendaji ya ‘’kurejesha imani katika mfumo wetu wa kisheria wa uhamiaji kukuza ujumuishaji wa wamarekani wapya.’’Agizo hili linaanzisha tena kikosi cha kazi kwa mmarekani mpya,ambayo ni pamoja na wanachama wa mashirika ambayo yanatekeleza sera zinazoathiri jamii za wahamiaji.Agizo pia linaelekeza mashirika kupitia sheria ya malipo ya umma ya 2019 ambayo unaweza kusoma zaidi juu yake kupitia kwa tovuti ya www.ilapmaine.org/public-charge . Agizo pia linahitaji wakala kupitia sera za hivi karibuni za uhamiaji ,huondoa kumbukumbu inayohitaji wafadhili kulipa serikali ikiwa mwanafamilia atapata faida za umma,na anaanza mchakato wa kukagua kurahisisha uraia.kujenga upya na kuongeza uandikishaji wa wakimbizi.Rais Biden alitoa amri ya mtendaji kujenga upya programu ya uandikishaji wa wakimbizi wamarekani na pia imejitolea kukuza kifungu [cap] cha wakimbizi hadi 125000 kuanzia oktoba.Aliamuru DHS kuzingatia kuhoji wakimbizi kwa mbali na kuelekeza serikali kuajiri maafisa wakimbizi zaidi .Agizo hilo lilitangaza kuwa utawala wa Biden utapana kipaumbele makazi mapya ya wanawake ,watoto na wengine wanaokabiliwa na mateso kwa sababu ya jinsia yao au mwelekeo wa kijinsia.Agizo pia linaelekeza mashiririka kuchunguza njia za kuwasaidia watu waliohamishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kuhusu sheria, utawala wa Biden umetangaza mswada mkubwa wa mageuzi ya uhamiaji unaoitwa sheria ya uraia wa Marekani ya 2021 [US Citizenship Act of 2021].Hata hivyo ,tafadhali ufahamu kuwa sheria sio sheria kwa sasa.Usimlipe yeyote anayekuambia kuwa atakusaidia kupata uraia kupitia mwongozo wa mswada mpya, kwa sababu sio waaminifu.Hakuna sheria mpya kwa sasa.Tutahitaji msaada wako katika siku zijazo kuwasiliana na ujumbe wa bunge la Maine kuhusu mswada huu na sheria nyingine. Pata mengi zaidi kupitia kwa tovuti ya https://www.ilapmaine.org/legislative-priorities.
Julia brown Esq ni mtetezi na mkurugenzi wa outreach [kufikia]wa ILAP.