naye Jean Damascene Hakuzimana

Korti ya katiba ya Burundi iliamua kwamba Evariste Ndayishimiye anapaswa kuapishwa kama rais baada ya kifo cha ghafla cha mwenye nguvu Nkurunziza, ambaye muhula wake ulitazamiwa kumaliza mnamo Agosti 2020. Warundi na marafiki wao wanaomboleza kifo cha ghafla cha Nkurunziza Jumatatu, Juni 8 kunako Hospitali la Cinquantenaire ya Karusi la Burundi.
Rais Nkurunziza alikufa kutokana na moyo kushindwa, kwa mujibu wa tangazo la Katibu Mkuu mnamo tarehe Juni 9. Tangazo hilo liliripoti kwamba Nkurunziza alikuwa akihudhuria mchezo wa mpira wa wavu Jumamosi, Juni 7 na alionekana akiwa mwenye afya nzuri, lakini baadaye afya yake ilidhoofika kwa haraka.

Changamoto za kisiasa zilikuwa katika muchanganiko kutaka kujua ni nani atachukua madaraka na kuendelesha baada ya Nkurunziza, ambaye alifariki karibu na mwisho wa muhula wake. Kulingana na Aljazeera, mahakama ya katiba ilisema kwamba kipindi cha mpito sio lazima, na kwamba rais aliyechaguliwa anapaswa kuapishwa mapema iwezekanavyo.

Mnamo Mei 18, Amjambo Afrika iliripoti kwamba wakati ulimwengu unajitahidi kudhibiti mkurupuko wa ulimwengu wa COVID-19, nchi iliandaa uchaguzi wa rais na wabunge ambapo umati wa watu na mikutano ilifanyika bila masks au mtengo wa kijamii. Mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni, vyombo vya habari vya kijamii vilimwonyesha Rais Nkurunziza – Mkristo mwenye bidii – akijitokeza kwenye mikusanyiko mingi ya Kikristo, akipunguza hatari zinazohusiana na hili janga. Katika chapisho moja lililo sambazwa sana, alisema kuwa COVID-19 hupita angani, lakini kwamba Mungu alikuwa ameitakasa hewa kiasi kwamba haiwezi kuwemo na virusi.

Gazeti the Guardian iliripoti kwamba baadhi ya vyombo vya habari vime taja rais kwamba anaweza kuwa ameambukizwa na Coronavirus mpya, ambayo hatimaye ilisababisha kifo chake cha mapema. Mke wake Denise Nkurunziza, ambaye alikimbizwa kwa ghafla Kenya kwa ajili ya huduma ya afya tarehe Mei 28, amerudi nchini Burundi baada ya kifo cha mumewe. Gazeti the Daily Nation liliripoti kwamba alikuwa akitibiwa kwa ajili ya COVID-19 na hali ya kimsingi

“Ikiwa inathibitishwa kwamba Rais Nkurunziza alifariki kutokana na ugonjwa wa coronavirus, ingeweza kuwa fundisho kwa viongozi ambao bado wanadharau kuchukulia ugonjwa huu hatua na wala hawasaidii watu wao kuudhibiti,” alivyosema mkimbizi toka Burundi ambaye sasa anaishi Concord, New Hampshire, na ambaye hakupata habari za asubuhi za tarehe Juni 9. Alisema kwamba amekuwa akizungumza na wanafamilia nchini Burundi ambao walimthibitishia kwamba serikali inachambua uchapishaji wa habari kuhusu COVID-19. Nkurunziza anaweza kuwa rais wa kwanza kufa kutokana na COVID-19, ili ripoti New York Post.