Mchapishaji Hariri Georges Budagu Makoko

 

Kama ilivyo wakati wa uandishi wa habari, bila kujuwa lini mwisho kabisa wa shida hii ya kiafya, watu 727,357 ulimwenguni wamekufa kutokana na ugonjwa coronavirusi mpya , na zaidi ya watu milioni 19.6 wamepatwa na ugonjwa wa COVID-19. Tunajua sote kuwa mgogoro huu unatishia ustawi wa kiuchumi wa watu binafsi na wa mataifa. Ikiwa pamoja na kuumiza na kuvuruga kwa mifumo ya elimu kokote ulimwenguni, na matokeo ambayo yanaweza kuhisi kwa kizazi, na labda zaidi.


Hakuna mahali pengine palipo wasiwasi kuhusu elimu kuwa kali zaidi kama ilivyo kwenye sehemu zilizo masikini sana ulimwenguni, zikiwemo nchi nyingi barani Afrika, ambapo watoto milioni 710 wamekatishwa shule, kulingana na Washirika wa Ulimwengu dhidi ya Elimu. Kwa dhiada, katika nchi nyingi za KiAfrika, shule haziwezi kumudu vifaa na teknolojia muhimu ili kuweka wanafunzi angalau kwa njia fulani kwenye shughuli za masomo wakati wamefungwa, na ambayo inamaanisha kuwa watoto wachache tu katika nchi zinazoendelea wanapewa anasa ya kusoma kwa mitambo ya mbali, kama vile watoto wanavyoweza kufanya nchini Marekani.


Hata nchi hilizomo barani Afrika ambazo zimejaribu kuunganisha waalimu na wanafunzi kupitia programu ya redio au Televisheni, au kwa kutumia programu za simu kama WhatsApp, zimeshindwa kufikia watoto wengi kwa sababu udogo wa miundombinu ya teknolojia. Hii imefanya elimu isiweze kufikiwa na walio wengi. Matokeo yaliyotarajiwa chini ya mstari ni pamoja na matarajio ya mripuko katika viwango vya kutojua kusoma na kuandika na kupungua kwa idadi ya wahitimu. Daktari Lazare Sebitereko, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Eben-Ezer nchini DR Congo, alinishirikisha wasiwasi mwingine: Kadiri vijana wanapokataliwa mbali kwa tumaini ambalo elimu inaleta, watavutiwa zaidi na kushiriki katika vikundi vyenye kushika silaha na wanaweza kutafuta ustawi wao kwa njia hiyo, na hivyo kuzidisha uharibifu chini barabarani kwa bara ambalo tayari limeathirika sana kutokana na vurugu.


Kua kukua nchini DR Congo, katika jamaa ya wazazi wasiojaliwa kupata elimu, nilikuwa na marafiki wengi ambao hawakuwahi kupata elimu. Wengi kati ya marafiki hawa wanaishi kwa sasa katika mazingira yenye kuathiriwa vibaya katika kijiji change cha kuzaliwa. Ijapo kuwa hawa walikuwa watoto wa akili sana. Ni mazingira na hali walio kua amo ndiyo imesababisha maisha yao ya baadaye na nini wange weza kutimiza maishani. Kwa upande wangu binafsi, nilichochewa na udadisi wa kipekee wa kutafuta elimu, na hali zilizo jipanga kwa faida yangu. Na kama matokeo ya elimu yangu, maisha yangu yalibadilika. Moyo wangu unaumizwa kwa ajili ya mamilioni ya watoto ulimwenguni kote ambao wataathiriwa sana na janga hili la sasa. Watu wenye moyo wa huruma, fadhili, na serikali wasinge paswa kuwasahau watoto hawa.


Labda hatupaswi kusahau somo kubwa zaidi kutokana na janga hili – kwamba sote tumeunganishwa. Kwa hivyo, kadiri ya rasilimali zaidi tunazoweka kando ili kusaidia mifumo ya elimu ulimwenguni kote wakati huu mgumu, kadiri hali nzuri zitakuwa pasipo wasiwasi kwa jamii zetu katika siku zijazo. Ushirikiano wa Kimataifa kwa ajili ya Elimu umekuwa ukifanya kazi kwa bidii sana ili kusaidia nchi zinazoendelea kwa vile zinajitahidi kupunguza athari ya inayo tokana na kufungwa kwa shule kwa watoto walio hatarini zaidi duniani. UNESCO imeunda muungano kwa sababu hiyo hiyo. Kulingana na UNESCO, “wanafunzi milioni 24 kutoka elimu ya msingi hadi elimu ya juu wapo hatarini ya kutorudia kwa mafunzo mwaka wa 2020 kufuatana na kufungwa kuliko tokana na COVID-19. Sehemu kubwa ya wanafunzi wako hatarini, milioni 5.9, wanaishi Kusini na Magharibi mwa Asia. Wanafunzi wengine milioni 5.3 walio hatarini wako katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Mikoa yote miwili hii ilikabiliwa na changamoto kali za kielimu hata kabla ya janga hilo, ambalo linaweza kuzidisha kufanya hali yao kuwa mbaya zaidi. ”


Hapa Marekani, mifumo ya shule iko inamwagia rasilimali katika kutoa habari moto moto kwa wavuti, milo ya bure, computer ya mkononi, na vifaa vingine kwa wanafunzi katika shule zao, wakiwa na matumaini kwamba vijana wanaweza kufuata elimu yao kwa usalama katika muktadha wa janga. Hata hivyo hapa pia, palipo na rasilimali kubwa zaidi kuliko katika nchi nyingi, watoto wamoja watapata shida ya ucheleweshaji katika elimu yao ambayo inaweza kuwaathiri kwa miaka ijayo. Hii ni pamoja na watoto kutoka katika familia za wahamiaji, ambao wazazi wao hawana rasilimali ya lugha au ujuzi wa utamaduni kusudi kusaidia watoto wao na kazi za shule kwa wakati ambao walimu wametengwa kuwa mbali sana na watoto wanaojaribu kuwahudumia. Kama wakiritimba, wasimamizi, na waalimu wanafanya kazi kwa ubunifu kujaribu kuunda sera na michakato ambayo itamfanya kila mtu salama na kujifunza, nawasihi uangalifu maalum uchukuliwe kwa watoto wa wahamiaji, na wengine kutoka familia ambao wanakabiliwa na vizuizi hapo juu na zaidi ya wale watoto wa waMarekani wa kawaida.


Kwa kawaida, mwezi wa nnane hapa Marekani huwa wenye shughuli nyingi, pamoja na jamii kutayarisha mwaka ungine wa shule. Ila wazazi wengi hutupwa katika ukosefu wa uhakika ulio tokana na janga hili. Hawajuwi namna gani mwaka wa shule utafanana, na miundo gani itakuwepo, Wazazi wahamiazi kwa upekee wamechanganyikiwa, wakikabiliana na ujoto wa kuogelea katika tamaduni mpya ya mwendo wa shule- na juu ya hiyo mwendo wa kukabiliana na matokeo ya Coronavirus. Wakati ambapo shule na bodi za shule zinajitahidi kuhudumia wanafunzi katika matunzo, tafadhali kutana nao. Wajulisheni watoto wenu wanahitaji nini ili kufanikiwa. Katika Marekani, utetezi wa wazazi unatazamia na pia unadhaminiwa.Na kwa sasa, zaidi ya hapo ilivokuwa, tunahitajika kutetea kwa faida ya watoto wote nw muundo wa majifunzo unao fanya kazi kwa ajili ya wote.