“Uhunga ikikwiruka inyuma ariko nduhunga ikikwirukamo.”
“Ni rahisi kukimbia kinachotokea nyuma yako, bali vigumu
kupiganisha kilicho ndani mwako”.

Georges Budagu Makoko, Amjambo Africa, Mchapishaji
Kathreen Harrison, Amjambo Afrika, Mhariri kiongozi

Virusi mbaya vya COVID-19 vimeambukiza watu katika nchi zaidi ya 200 na ma wilaya, na kuharibu maisha, kutisha watu, na kuharibu uchumi. Mnamo tarehe Machi 12, Maine ilithibitisha kesi yake ya kwanza ya COVID -19, iliyo ifanya iwe serikali ya 43 iliyo ambukizwa. Gavana Janet Mills mara alitangaza kwa haraka hatua za bima za dharura ili kusaidia wakaaji wote wa Maine kupata huduma za afya zinazohusiana na virusi, pia ametoa pendekezo iliyo na lengo la ku sawazisha mkunjo, na kupatia bahati huduma ya afya nafasi ya kujiandaa kupokea wagonjwa wa COVID-19. Mkurugenzi wa Kituo cha Maine cha Udhibiti wa Magonjwa, Dk Nirav Shah, hutoa sasisho za kila siku kwa umma ili kuwasaidia wakaaji wa Maine kuelewa na kujibu kwa tatiso hili linavyoendelea. Mnamo Machi 27, hesabu za kesi huko Maine ziliongezeka hadi 168, na Maine ili rikodi kifo cha chake cha kwanza kutokana na Covid-19, alikuwa mzee katika umri wa miaka yake ya 80.

Viongozi wa wahamiaji wamejitahidi sana kusaidia washiriki wa jamii zao na kuwapa mara kwa mara habari juu ya jinsi bora ya kulinda afya na usalama wa familia zao, na pia kwa jamii zao kwa jumla. Habari juu ya dalili zinavyojitokeza, hatua za kuchukua ili kuzuia kusambaza vijidudu, na nini cha kufanya ikiwa kesi inatuhumiwa hivi viimetafsiriwa kwa lugha nyingi tofauti ili kila mtu aweze kuelewa. Vikundi vya jamii vimeunda sehemu ndogo za video katika lugha nyingi ili kushirikisha sasisho mpya na wanamemba wao kupitia WhatsApp, Facebook, na majukwaa mengine kama Amjambo Afrika ili kuwafikia wale ambao hawafuati vyombo vya habari vya habari vinavyotawala.
Amjambo Afrika ina kitufe kipya cha Covid-19 kwenye tovuti yake ambayo inaelekeza wageni kwenye habari kwa Kifaransa, Kiswahili, Kireno, Kisomali, na Kinyarwanda. Baadhi ya habari hizo zipo katika mfumo wa video kutoka kwa jamii wanamemba wanaojulikana, nyingine ni katika maandishi au katika michoro ya habari. Tunakuhimiza kutembelea tovuti hii na kuishirikisha sana kwenye mitandao yenu. Habari zetu ni za msingi kwa sasisho kutoka kwa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa, Shirika la Afya Ulimwenguni, na viongozi wa jamii wa hapa. Tunatoa habari kwa mikutano ya waandishi wa habari ya kila siku, kwa kukutana na idara tofauti za serikali, kama Idara ya Kazi, na Idara ya Afya na Huduma za Binadamu, na vikundi mbalimbali vya wafanyakazi vinavyoongoza mbele.

Utamaduni, imani, na uzoefu wa zamani vyote pamoja huchukua jukumu muhimu kwa njia ambayo kila mtu na jamii tofauti wanavyo shughulikia nyakati za hatari. Baadhi ya wahamiaji wengi waliowasili hivi karibuni huko Maine walitoroka vitisho vingi nyumbani walikotoka – Na ndiyo sababu wako hapa. Mwanzoni, COVID-19 inaweza kuwa isiwashtushe haraka kama inavyo waogopesha Wamarekani wengine ambao wameokolewa vita kwenye ardhi yetu, na milipuko ya magonjwa kama Ebola, Malaria na Kifua Kikuu. Walakini, wakati uwingi wa yale yaliyokuwa yakifanyika yalionekana kuwa wazi, kiwewe ambacho wengi wao waliyo pitia katika nchi zao, na kwa safari yao kuja Maine – mahali walitarajia itawapa usalama – kilisababishwa tena na janga hilo.

Wakati habari za virusi hivi zilipogonga masikio ya watu wa Maine, walienda mara moja kwenye ma duka na kununua bidhaa zote za kusafisha mikono na kusafisha nyumba. Kufikia wakati wahamiaji walipogundua kiwango cha shida hii waligadhabika kuona bidhaa nyingi muhimu zimepotea kutoka ma duka. Kwa vyovyote vile, na kama walivyo watu wa Maine wenye mapato ya chini, wahamiaji wengi huishi kwa kulipa kutokana na waliolipwa, na hivi hawawezi kununua na kuweka ghalani chakula kwa mawiki kadhaa, na wana wasiwasi kwamba si kila mtu atapata bahati sawa kujitoa katika shida hii.

Kusambazwa kwa COVID-19 ni ukumbusho kwamba sasa tunaishi katika kijiji kilichounganika ulimwenguni – yaani kinachotokea mahali mbali na sisi kinaweza kutufikia kwa urahisi na haraka na kuhatharisha sana maisha yetu. Na kama ilivyo katika maisha ya kijijini, tunahitaji kujaliana, na kugawana rasilimali, ili asiye na mapato ya kutosha miongoni mwetu asiteswe sana.

Amjambo Afrika inayo matumaini kwamba jamii zetu zote – waliozaliwa ugenini na wale waliozaliwa hapa – watatii ushauri wa wataalam na kubaki nyumbani muda wote na kwenda inje tu ikiwa kkuna jambo muhimu, kuosha mikono kwa nguvu mara kwa mara, kufunika kikohozi na chafya, kutakasa mahali na pahali, na kujuiana hali mmoja na mwengine . Pamoja tunaweza kupunguza kusambazwa kwa virusi vya COVID-19, na hivyo kutolea vituo vya matibabu nafasi ya kuendelea kushugulika na kesi za watu wanaougua, na wanasayansi kujitahidi kuunda chanjo kinyume cha virusi hivi.

Tukiamini kuwa amani ya akili na utulivu vitaundwa katika serkali la jimbo letu mara moja kabla haijakuwa nyuma zaidi, tunawatakieni bora marafiki zetu.