Akryoshe nti gahera mwitama
“Something sweet does not last a long time in your mouth”

Kitu kitamu hakidumu kinywani mwako
Katika jumuiya za wahamiaji kutoka Afrika, harusi ni makusanyiko makubwa zaidi ya kijamii. Washiriki hutumia muda pamoja, wakifurahia mzunguuko wa mila, mavazi, na tabia, na kuchangia pamoja chakula chenye ladha. Kila kitu juu ya harusi ni ya kuvutia na kuchamusha mioyo ya wale wanaohudhuria. Kiasi kwamba hata wale wasioalikwa hutaka kuwa hapo! Katika baadhi ya nchi za Afrika sherehe za harusi huchukua siku nyingi hali kila mtu akifurahia kuwa pamoja na mwengine na kushiriki katika sherehe.
Watu wa Afrika waliopo hapa nchini Marekani wanasafiri kwa gari au kulipa nauli ya ndege kwa mamia au hata maelfu ya maili ili kwenda kushiriki harusi ya familia na marafiki. Wengine huja kutoka Afrika, Ulaya, Australia au mahali pengine pote pale ili kushiriki harusi. Hapa Maine idadi ya watu wanao hudhuria harusi ya kiAfrika inaweza jumuishwa kati ya watu mia tatu na tano. Bajeti ya harusi ni kubwa na huendesha kati ya dola kumi na mbili na kumi na tisa elfu kwa harusi ya wastani. Kwa watu wenye misingi imara, kiasi ambacho hutumiwa ni mara zaidi.
Maandalizi ya harusi huchukua muda mkubwa kwa kipindi cha miezi isiyo michache. Kamati na kamati ndogo hukutana mara kwa mara kabla ya harusi ili kuweka mipango ya kazi tofauti: kama namna ya mapambo ya maua; kupanga mipaka kwa kuwakaribisha waalikwa kulingana na hali ya familia au jamii; kutayarisha nyumba kwa wageni katika nyumba za wale waliojitolea katika jamii; gharama za usafirisaji; harambee. Fedha ya kusaidia kulipa ndoa hutokea kwenye mchango katika jumuiya na kote nchini na hata katika mabara. Ni kawaida sana wakati mtu anakuwa na harusi hapa Maine kuingiza marafiki na familia kutoka Ulaya, Australia na Afrika. Wote hawa walioalikwa kuja kwenye harusi na pia kusaidia kuunga mkono harusi kifedha. Kuna ununuzi mkubwa ghafla ya tiketi, uhamisho wa fedha, na uingizaji wa gharama za harusi miezi kabla ya harusi.Teknolojia na vyombo vya kusambaza habari vya kijamii vimeifanya iwe rahisi kuunganisha watu kutoka pembe tofauti za dunia.
Marafiki waAmerika ambao wamehudhuria ndoa za kiAfrika wanasema wanavutiwa na mila inayohusishwa na harusi. Ikiwa harusi ni ya Mkristo, huduma za kanisani ni ndefu na mara nyingi huanza nyuma sana. Mabadilisho ki asili kati ya familia ya bwana na ya bibi harusi kwenye eneo ya mapokezi huendelea kwa muda mrefu. Ngoma za jadi ni za kushangaza na za burudani. Familia ya ndoa hujitahidi kutengeneza chakula cha ladha zaidi iwezekanavyo ili ku furahisha wageni wa heshima – familia ya bibi arusi. Harusi ya Kiislamu huingiza mila ya kidini ambayo ni tofauti na mila ya Kikristo. Kwa Waislam sehemu ya kidini inafanyika nyumbani na mkusanyiko mdogo ambao ni pamoja na kuweko kwa Imamu. Imamu husaidia katika kutekeleza mkataba wa ndoa. Baada ya hii huja karamu kubwa ya jamii. Tuseme kwamba kwa jamii zote za Afrika, harusi huendeshwa kwa masaa au hata masiku.
Kwenye hatua hii na kwa wakati huu hapa Maine kuna ndoa kadhaa zenye mchanganyiko kati ya Waafrika na Wamarekani. Ikiwa kweli, ndoa zilizochanganywa kati ya jamii tofauti za Afrika pia ni chache. Waislamu huwa hawakubali kuoa Wakristo, na vivyo hivyo, lakini pia si kawaida kwa Waafrika kutoka kwenye utamaduni mmoja kuoa Waafrika kutoka kwa mwingine. Hapo awali, katika jamii nyingi za Kiafrika, ndoa ilikuwa inaandaliwa na wazazi, lakini siku hizi tulimo wanaotaka kuowana wanajiamua wenyewe kuowa na kuolewa. Hata hivyo bado wanatafuta idhini kutoka kwa wazazi. Kwa kawaida wazazi wa Bibi arusi wana mengi ya kusema juu ya uchaguzi wa mume kwa kuwa wanataka kuwa na hakika kwamba binti wao hatateseka katika ndoa. Tofauti moja kubwa kati ya harusi za Afrika na Amerika zinazoendelea ni jadi ya kutoa dowari/mali kwa wazazi wa msichana. Dowari/mali inaweza kuwa dhahabu, fedha, wanyama kama mbuzi au ngamia, au zawadi nyingine za thamani
Majirani ya familia wanaofanya harusi wataona haraka sana vurugu kubwa kujitokeza kandokando ya nyumba zao. Wao wataona harakati kubwa ya watu wanaoingia na kutoka nje ya nyumba pia magari kuegeshwa karibu na barabara masaa marefu kwa siku chache kabla na pia baada ya harusi yenyewe. Baadhi ya Waafrika wamejifunza kujuwa kwamba ni wazo nzuri kuwajulisha majirani zao wa mitaa kuhusu harusi ijayo ili kuepuka kuwatisha au kuwafadhaisha kwa harakati isiyojulikana ya watu katika ujirani.
Ndoa na arusi zina jukumu muhimu sana katika maisha ya tamaduni zote, ikiwa ni pamoja na utamaduni wa ndani wa kimarekani wa sasa. Hakuna ukubwa wa kawaida wote linapokuja suala la utaratibu wa wanandoa. Taratibu zinatofautiana kwa hesabu ya watu wanaohusika, gharama zinazohusika, dini, desturi na mila.
Amjambo Afrika! inawahimiza wasomaji wetu kujifunza kuhusu desturi za ndoa za tamaduni za watu wengine. Na tafadhali – ikiwa una picha ya harusi ambayo ungependa tuingize katika toleo la baadaye, uitume kwa [email protected]