Dalili zifuatazo zinaweza kuonekana siku 2 hadi 14 baada ya kufichuliwa. *

  • Homa
  • Kikohozi
  • kupumua kwa shida

 

Magonjwa yaliyoripotiwa yame pangwa kuanzia dalili dhaifu hadi magonjwa kali hadi kifo kisha kuthibitishwa kwa coronavirus 2019 (COVID-19). Hadi sasa hakuna chanjo lolote lile la kujikinga na ugonjwa wa coronavirus 2019 (COVID-19). Njia bora ya kujikinga  na maradhi ni kuepuka virusi hivi. Virusi hivi vina ambukizwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu mwengine.

 

Hapa chini kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kujikinga, kukinga familia yako, na jamii.

  • Osha mikono yako mara kwa mara na sabuni na maji kwa sekunde 20, haswa baada ya kwenda chooni; kabla ya kula; na baada ya kutoa kamasi kwa pua yako, kukohoa, au kupiga chafya. Ikiwa sabuni na maji hazipatikani kwa urahisi, basi tumia sanitizer iliyo na kiasi cha alcohol angalau 60%.
  • Epuka ku karibiana na watu ambao tayari ni wagonjwa.

 

  • Epuka kugusagusa macho yako, pua na mdomo.

 

  • Kaa nyumbani ukiwa u-mgonjwa.

 

  • Funika kikohozi chako au kupiga chafya na karatasi-tishu, kisha tupa tishu hiyo kwenye kapo la takataka.

 

Safisha na Takasa mara kwa mara vitu vilivyoguswa na maeneo yote kwa kutumia dawa ya kawaida ya kusafisha nyumba kwa kufukiza au kufuta.

 

  • pazia ya usoni inapaswa kutumiwa na watu ambao wanaonyesha dalili za magonjwa COVID-19 ili kusaidia kuzuia kusambazwa kwa ugonjwa huo kwa wengine. Matumizi ya pazia ya usoni pia ni muhimu kwa wafanyakazi wa afya.

 

Wazee wanapaswa kujaribu:

 

  • kuepuka maeneo ya umma na umati wa watu
  • kukaa nyumbani kadri uwezavyo
  • kuepuka kusafiri baharini na safari ndefu angani kwa ndege

 

Tuwasaidie walio wanyonge na hatarini kwa kuwazuia kuenda maeneo ya watu wengi – hii ni pamoja na wazee au wale walio na hali sugu ya kiafya kama ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa sukari, na ugonjwa wa mapafu. Fikiria kuwanunulia vifaa dukani na kwenda hapa na pale kwa ajili yao.