By Kathreen Harrison

Photo | John Ochira

 

Shida la Covid-19 limehatarisha maisha kwa mamilioni ya watu ulimwengu kote, ikiwemo jamii za wahamiaji wa Maine. Watu wamepoteza kazi, shule zimefungwa, tamasha za kitamaduni na maadhimisho yamefutwa, huduma za ibada zimepeperushwa hewani, na neno “umbali wa kijamii” limeingia katika msamiati na hata kwa wale walio wasemaji wapya wa Kiingereza.
Ili kukabiliana na shida hilo, mnamo Machi 13, Mufalo Chitam, mkurugenzi wa Shirikisho la Haki za Wahamiaji wa Maine (MIRC) na Inza Ouattara, Mratibu wa Afya wa Wakimbizi kwa Shirika la Catholic Charities la Maine, waliitisha mkutano kwa njia ya simu na viongozi wa jamii za wahamiaji wa Maine pamoja na wahusika wa afya ya umma kwenye Kituo cha Uchungunzi wa Magonjwa (CDC) Kristine Jenkins na Jamie Paul ili kujadiliana kuhusu janga la sasa la coronavirus na kuanzisha njia madhubuti ya mawasiliano kati ya wanachama wa jamii za wahamiaji na Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa (CDC).
Mkutano huo ulihusika na miongozo ya sasa ya CDC kwa usalama wa umma, na wale waliohudhuria waliombwa kutumia njia zao za mawasiliano ili kupata kutekelezwa kwa miongozo ifuatayo katika maeneo yao kwa haraka iwezekanavyo:
• Osha mikono na sabuni na maji kwa nguvu mara kwa mara kwa angalau sekunde 20, ukizingatia sana migongo ya mikono, katikati ya vidole, chini ya kucha za vidole.
• Tumia sanitizer inayotengenezwa kwa alcohol kwa kusafisha mikono ikiwa maji hayapatikani
•Baki nyumbani ikiwa u mgonjwa
• Funika kikohozi na kupiga chafya na tishu kisha utupe mbali tishu hiyo
• Epuka kusafiri
• Pigia daktari simu ili kuripoti dalili mbaya (kama vile homa, upungufu wa pumzi, ugumu wa kupumua) badala ya kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha dharura au kwa ofisi ya daktari.
Kuzoea kukaa kwa umbali wa kijamii kwa kujitenga kwa miguu 6 na wengine, zaidi sana kwa wazee na watu wenye matatizo makubwa ya kiafya; kuendesha mikutano kwa njia ya hewani; kuzuia umati wa watu. (Na zaidi ya hayo njia za kujizuia kuambukizwa virusi kutoka kwa wengine, umbali wa kijamii unatarajiwa ili kupunguza kasi ya kusambazwa kwa virusi, na kuruhusu hospitali na wauzaji wa vifaa vya matibabu kuzingatia mahitaji. Kutokana na data ya miaka 100 ya afya ya umma, umbali wa kijamii ni ufunguo halisi wa kudhibiti kasi ya maambukizi kwa sababu virusi husambazwa kwa njia ya mawasiliano ya karibu na mtu ambaye ameichukua. Mawasiliano ya karibu inajumuisha mtu kuwa kati ya mita 2 (miguu 6) karibu na mtu angalau kwa dakika 15. Mtu anaye beba ugonjwa anaweza kuwa haonyeshi hata dalili za ugonjwa. Ila watoto mara chache huwa na dalili kali. Walakini, kupiga chafya, kukohoa, na hata kuongea husambaza matone angani ambayo yanaweza kuvutwa kwa pumzi. Kwa wakati huu hakuna ushahidi wowote kwamba virusi hivi husambazwa kupitia chakula).

 

Photo | John Ochira

Zaidi ya miongozo ya jumla, mkutano huo ulilenga kubaini maswala yanayoweza kuwa ya muhimu kwa idadi ya wahamiaji. Hii ni pamoja na uhitaji wa nyenzo katika tafsiri tofauti ili wale walio wageni kwa Kiingereza waweze kuelewa virusi, jinsi vinavyosambazwa, na jinsi ya kujizuia kuambukizwa.
Kufuatana na mkutano wa Machi 13, vyama vya jamii na mashirika yasiyo ya faida walifanya kazi kutengeneza na kukusanya video na vikaratasi vilivyo andikwa katika lugha mbalimbali zinazoelezea juu ya dharura ya kiafya. Vifaa hivyo vinashughulikia mada nyingi, pamoja na jinsi virusi vinavyoambukizwa, nini maana ya ‘kutengwa kijamii’, kufutwa kwa shule, hadithi zinazosemwa juu ya virusi, umuhimu wa kutafuta njia za kusalimiana badala ya kushikana mikono na kukumbatiana, na kwanini watu wana hitajika kubaki nyumbani kila ikiwa inawezekana.

Mbali na kutia vifaa hivyo kwenye tovuti mbali mbali kama Amjambo Afrika, mashirika yameya peleka mbali kupitia social-media na WhatsApp. Zaidi, zikionyesha hitaji la kufikia watu mmoja kwa mmoja, ili kuwasiliana kwa njia sahihi za kitamaduni, vyama kadhaa vya jamii ya wahamiaji wameenda mlango kwa mlango nyumbani ili kushirikisha jamii zao habari muhimu za kiafya. Viongozi wameripoti kuwa nyenzo zilizotafsiriwa zimefikia jamii zao, na sasa wengi wao wanafuata miongozo iliyoko.

Coronavirus mpya Covid-19 imeingia tayari kwa nchi 188 au wilaya, na sasa iko inaenea barani Afrika, ambapo nchi 40 zimeripotiwa kesi 572 zilizothibitishwa, na vifo 12, tangu ilipofika Machi 21. Maswala mbalimbali kuhusu kwa nini kiwango cha maambukizo kilikuwa bado chini sana barani Afrika ni pamoja na hatua ambazo zilizokuwepo kwa sababu ya uzoefu wa awali wa bara hili na magonjwa mengine kama Ebola.

Photo | John Ochira

Kulingana na Profesa Jean-Jacques Muyembe, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Biomedical (INRB) huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hatua hizo hizo zilizolinda dhidi ya Ebola zinaweza pia kulinda dhidi ya Covid-19.

Katika nakala ya Februari 20 kwenye tovuti la Shirika la Afya Ulimwenguni, Muyembe alinukuliwa kuwa alisema, “Tangu milipuko wa 10 wa Ebola, hata majimbo yaliyo kuwa hayakuwa na kesi yameweka mifumo ya kuwachunguza wasafiri na kukuza uoshaji wa mikono, na hatua hizi ndizo zinahitajika kwa kupiganisha coronavirus. ” Aliongeza kuwa kwa sababu ya Ebola, nchi imeazimisha mfumo wa maabara ambao sasa unaweza kutumika kwa kupima ugonjwa wa coronavirus pia. Walakini, tofauti na Ebola, wanao ugua ugonjwa mkali wa Covid-19 wanahitaji mashini ya usaidizi wa kupumua, na hizi ni haba kutolewa katika nchi nyingi, ikiwemo DRC.

Kulingana na CNN, hatua zingine zinazochukuliwa barani Afrika kupunguza kasi ya usambazaji wa virusi ni pamoja na kuwekwa kwa vifaa vya kuoshea huko Kigali, Rwanda, ambapo abiria wanalazimishwa kuosha mikono kabla ya kupanda ndani ya basi; kila mtu anashurutishwa kupimwa homa na kutumia wasanifu wa mikono kabla ya kuingia kwenye nafasi za umma huko Lagos, Nigeria; vizuizi vya kusafiri vimewekwa katika nchi nyingi.

Photo | John Ochira

Wazo hilo lilizunguka kwa muda mfupi barani Afrika na Amerika kwamba watu weusi hawawezi kuambukiza Covid-19, hata hivyo kusambazwa kwa virusi hivi barani Afrika, na vile vile kesi za hivi karibuni miongoni mwa watu mashuhuri nchini Marekani, pamoja na zile za watu wawili wa asili ya kiAfrika wachezaji wa mpira wa kikapu NBA zimenyamazisha fununu. Hadithi zingine bado zinazunguuka zikiwemo na wazo kwamba kugogoma maji mavuguvugu pamoja na chumvi huua virusi; kwamba supu ya pilipili na fennel ni kinga dhidi ya virusi; kwamba kikausha nywele huua virusi, kwamba virusi hastawi vizuri katika hali ya hewa ya joto. Hadithi hizi zote zime futwa mbali.

Maswali yaliyopo bado katika akili za viongozi wa wahamiaji na washirika wao ni pamoja na ikiwa upimaji wa COVID-19 utakuwa kwa bure kwa wanaotafuta hifadhi; jinsi gani watu walio na kipato kidogo wanaweza kupata vifaa vya kutosha ndani ya nyumba zao, kama vile chakula, karatasi ya choo, wasanifu wa mkono, dawa ya kuagiza, diapers; msaada gani utakaotolewa ili kuzuia wapangaji wasitupwe nje ikiwa hawawezi kulipa pesa ya upangaji; jinsi gani wafanya kazi wasio bado na kibali na wasio kwenye mipango ya usaidizi wa serkali watasaidiwa. Amjambo Afrika itaripoti majibu kwa maswali haya wakati watakapo ya pata. Tafadhali angalia Orodha za Huduma kwenye ukurasa 16, 20/21.

Angalia kitufe cha Covid-19 kwenye amjamboafrica.com kwa video, vikaratasi juu ya vilivyopo, na vifungu kuhusu virusi kwa Kifaransa, Kireno, Kisomali, Kiswahili, na Kinyarawanda. Tunapanga kujumuisha lugha nyingine zaidi kwenye tovuti letu hivi karibuni ili kuwasaidia walio na Kiingereza kidogo kwa kupata habari kadiri shida inavyoendelea.