4 women learned to ride a bike during the Bikes for All Mainers program, completed the final ride, and earned bikes to ride home and keep! Photo by Ainsley Judge

Baiskeli kwa wakazi wa Maine – mpango pasipo malipo kwa watu wakubwa wanaotafuta usafiri wa bei nafuu humu Portland – unakaribia kukomesha msimu wake wa 2019. Mpango huo unaendeshwa kwenye kitovu cha vifaa cha Portland pia hutolewa kwa kushirikiana na Umoja wa Baiskeli wa Maine. Wanafunzi wanaohusika katika mpango huo hujifunza ujuzi wa msingi wa matengenezo ya baiskeli na ufahamu juu ya uchukuzi. Zaidi ya hayo, wale wanaomaliza kozi ya saa sita (vikao viwili vya masaa matatu kila mmoja) hupata baiskeli inayo fanya kazi kikamilifu, iliyofanywa upya, ikiwa pamoja na kofia mpya na vifaa vya usalama.
Baiskeli kwa wakazi wote wa Maine ni mfano mzuri wa mema yanayo weza kutokea wakati mtu atambua haja ya ndani, anafikiri juu ya suluhisho, na kisha kuendea mashirika yasiyo ya faida ili kupata usaidizi. Nathan Hagelin ametambua miaka mitano iliyopita kwamba wengi wa wakazi wapya hapa Portland walikuwa wana gharamiwa zaidi juu ya usafiri, ao kutembea mwendo wa mbali ili kuenda kazini, madarasa yao ya kujifunza Kiingereza, mashirika ya huduma za jamii, na maeneo mengine hapa na pale mara nyingi hupatikana katika maeneo mbalimbali ya mji. Pia alijua kuwa wakazi wa Maine wengi wanazo baiskeli za ziada, zisizotumika zinazopatikana katika ghala zao na nyumba za chini ya ardhi. Aliwaendea Katibu wa Elimu na ufikiaji Shannon Belt, Meneja wa Umoja wa Baiskeli na kitovu cha vifaa cha Maine na Meneja wa Duka la Portland, Jaji Ainsley pamoja na wapendaji baiskeli watatu wakaamua kusaidia kutatua changamoto ya usafiri. Walizindua mpango wa Baiskeli kwa Wakazi wote wa Maine, ambao sasa umeingia kwa mwaka wake wa tano. Mpango huo hutoa baiskeli, na pia huhimiza maisha ya afya njema, hupunguza uchafuzi wa hewa wa ma gari katika mji, na tena hufundisha ujuzi wa usalama wa baiskeli ili waongoza ma gari na waongoza baiskeli wanaoshiriki barabara, wote wawe salama.
Shukrani kwa fedha mpya kutoka Benki ya Akiba Bangor, na fedha inayoendelea kutoka Umoja wa baisikeli wa Maine, mpango huo utahudumia wanafunzi 50 mwaka huu – kutoka 36 mwaka jana. Msimu wa 2019 utaanza Aprili tarehe 29 na kuendelea hadi mapema Agosti. Mafunzo yatafanyika katika madarassa ya kitovu cha vifaa cha Portland kilichoko kwenye anuani 85 Anderson St, na pia barabarani. Wakazi wa Maine wanaohitaji kushiriki lazima wawe na umri wa myaka 18 ao zaidi ifikapo wakati wa kuanza mafunzo, wakionyesha uwezo wa kupanda baiskeli, na kurudisha maombi iliyojazwa kwa Kitovu cha vifaa cha Portland kunako anuani 155 Washington Ave kabla ya wakati wa mafunzo. Maombi ya kushiriki mpango huu yanapatikana kwenye mtandao wa Kitovu cha vifaa cha Portland : https://portlandgearhub.org/bikes-for-all-mainers/
Kitovu cha vifaa cha Portland, ambacho hutoa ma baiskeli yote kwa mpango wa ma Baiskeli kwa ajili ya Maine, inatafuta wafadhili walio tayari kujiandikisha kwa kutoa baisikeli kwa wahudhuriaji wa msimu huu. Baiskeli zote zitafanywa upya na watengenezaji na wanaojitolea katika Kitovu cha Portland .
Baiskeli zinaweza kuletwa wakati wa saa za kazi kwenye duka la kitovu cha Portland kunako 155 Washington Avenue, Jumatatu hadi Ijumaa 4 za asubuhi – 12 jioni. na Jumamosi saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Misaada yote ni njia ya kupunguza kodi inayotokana na kodi. Mchango wa fedha pia unakaribishwa.