Kwenye makala yetu yaliopita, tumezungumza kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya kibinafsi. Mwezi huu tutaongea kuhusu njia za kufaidika kifedha unapofanya hivyo. Yafuatayo ni maoni machache kuhusu njia za kupunguza malipo ya bima:

• Malipo ya kujiendesha ama otomatiki. Wengi zaidi kati ya wenyeji wa bima watawapunguzia wateja wao wanapotia saini kwa malipo ya mara kwa mara, iwe ya kila mwezi, ama baada ya miezi mine, ama ya kila mwaka.Kampuni hupana kipunguzo hicho kwa sababu wanaweza tumia juhudi nyingi na pesa wakijaribu kujadiliana na wateja ambao malipo yao yamechelewa na sera zao zimo hatarini ya kufutwa kwa sababu ya kutolipa. Kwa hio kampuni zinataka kuhamasisha wateja wao kuchagua malipo otomatiki na hivyo sera za punguzo.

• Telematiki. Wenyeji wa bima wengi kwa sasa wanatoa teknolojia ambayo inafuatilia tabia za kipekee za dereva-tabia kama vile kasi, kusimama,saa gani ya siku dereva huendesha gari. Kulingana na utendaji, data hii inaweza kupungua kiwango cha bima cha dereva huyo, au kutoa marupurupu.Telematiki ni njia moja rahisi ya kulinganisha viwango vya bima ya gari a tabia binafsi za kila dereva na inaweza kupunguza haraka kiwango cha mteja-wakati mwingine kwa 25%. Teknolojia ya telematiki imeboresha kwa miaka ya hapa karibuna wakati mwingine inaweza kuingizwa katika program tumizi ya simu mahiri

• Kuunganisha sera. Wenye bima hutoa punguzo -na huduma bora- kwa wateja wenye laini zote za bima. Kuwa na bima ya gari pamoja na bima ya mali(iweya nyumba ama ya wapangaji) kwa kampuni moja ya bima inampatia mteja punguzo kubwa kwenye sera zote.

• Bima ya awali. Urefu wa bima ya awali unatoa akiba juu ya sera za bima iwe ya gari ama ya mali , kufuatana na mwenyeji wa bima hiyo.Kwenye kampuni zimoja, mteja akiwa na bima ya gari kwa muda mrefu, itamletea manufaa ya kiwango kizuri zaidi cha bima .Mteja yeyote anapopata nukuu mpya ya bima ya gari –ama bima ya mali- ahakikishe kwamba wakala ama mwenye kusimamia kampuni ya bima anaelewa vizuri ni miaka na miezi mingapi mteja huyo amekuwa na bima.Inatakikana hii bima iwe bima endelevu ili kuomba faida hiyo, bila mapumziko au upungufu wowote.