Naye Jean Damascene Hakuzimana

Nchi kadhaa barani Afrika zimeripoti idadi ndogo ao upungufu wa kesi. Hizi ni pamoja na Rwanda na Kenya, kutokana na New Times ya Rwanda ikiripoti kufunguliwa tena kwa safari za ndege za kibiashara ifikapo Agosti tarehe 1 na Kenya Airways inayo panga kuanzisha misafara ya ndege za ndani mnamo Julai tarehe 15. Tunisia inayotegemea utalii itafungua mipaka yake ifikapo Julai 27 kadiri nchi itavyoona hesabu za kesi za COVID-19 kuendelea kupungua. Na hesabu za kesi huko Algeria, Tunisia, Moroko, na Rwanda ziko chini sana kiasi kwamba Jumuiya ya Umoja wa Ulaya imetangaza taratibu za kuondowa vizuizi vya kusafiri kwa nchi hizo – Hiyo si kwa Marekani, ambayo raia wake wanazuiliwa kwa sasa kusafiri katika Umoja wan chi za Ulaya. Nakala ya hivi karibuni ya Amjambo Afrika ili husu “kuongezeka kwa Kesi za COVID-19 kwenye Bara la Afrika- kwanini na vipi?” iligusia kusema kwamba utamaduni wa kufuata amri za serikali zilizoenea barani Afrika zinafaa tu kwa nchi fulani za kiAfrika wakati huu.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayoshugulika na janga la Ebola ulipongezwa kama mfano ambao nchi nyingine zinaweza kutaka kunakili katika kupiganisha COVID-19 kutokana na kipengee cha maoni cha tarehe Juni 25 kilichoandikwa na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Daktari Tedros. Tedros Adhanom Ghebreyesus kwenye jarida the Guardian. Iliyopewa kichwa “Virusi havipumuziki. Ulimwengu unaweza kujifunza kutokana na jinsi DRC inavyo shinda Ebola, “Daktari Tedros aliandika kwamba kwa sababu watu wa Kongo waliamini sayansi, jamii, data, na ushirikiano na taasisi za kimataifa, taifa limefanikiwa kuwa karibu na kushinda Ebola. Alisema kwamba uzoefu wa DRC na Ebola umeiandaa nchi kuchukua sasa hivi hatua madhubuti za kinga.

Hapa karibuni, aliye apishwa kuwa Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameuzindua mpango “Sitaambukizwa na kueneza COVID-19” kulingana na jarida Associated Press. Hii ni tofauti kabisa na mtangulizi wake, ambaye hakujali ugonjwa huo hadi kifo chake cha hivi karibuni, kilicho daiwa kutokana na COVID-19. Wakimbizi wengi na waomba hifadhi kutoka Burundi wanaishi Maine. Wamesikitishwa na idadi ya vifo vya COVID-19 nchini Burundi, kwa hivyo habari isemayo kwamba rais mpya anachukua hatua juu ya ugonjwa huu huleta unafuu wa kukaribishwa.

Aljazeera imeripoti kwamba Afrika Kusini haifanyi vizuri, na ya kwamba nchi hiyo inahesabiwa asilimia 40 ya kesi zote zilizothibitishwa barani Afrika. Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kimeripoti zaidi ya vifo 4,079 nchini Afrika Kusini. Rais Ramaphosa ameonekana kwenye televisheni ili kutangaza wakati wa kurudi nyumbani wakati wa usiku, na pia marufuku ya mauzo ya pombe, hatua zote mbili zikikusudia kuzuia ajali, na kuhifadhi vitanda vya hospitali kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19. Ameamuru kuvaa vinyago vya uso.

Nchi barani Afrika zimo katika hatua za pamoja ili kuunda njia ya kutazama pamoja shida za kiuchumi zilizo sababishwa na janga hili. The Global Citizen imeripoti kwamba viongozi wa Afrika ya Magharibi waliahidi kiasi cha dolla millioni 25. Kama jibu ya mkoa huo kwa COVID-19, iliyokusudiwa ili kusaidia elimu, utunzaji wa afya, na ufikiaji wa usafi, miongoni mwa mipango mingine katika Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Africa ya Magharibi-ECOWAS