Siku nyingine nilihudhuria sherehe ya kuingizwa katika taifa hapa Portland,  kwenye Shule ya Kati iitwayo King. Watu arobaini na sita wa umri wote, dini na jamii – wanaume na wanawake pamoja na vijana – kutoka nchi 31 tofauti – kutoka Canada hadi Angola – walichukua kiapo ngumu kwa kufanya kuwa raia wa Marekani.

Wamoja walifika kutoka nyumba maridadi katika nchi za kidemokrasia. Wengine walikimbia vita, udhalimu na unyanyasaji.

Sasa wote ni majirani zetu, marafiki na wafanyakazi wenzetu. Wanaishi na hufanya kazi karibu mu ma kata zote za Maine. Wanalea familia zao na kwenda ku shule hapa  wakitumia vipaji na utaalamu wao kwa nchi ambayo inavihitaji sana.

Dr King nafikiri angependa kuwakaribisha. Na angeweza kutuambia kuwawapenda  kama tunavyowapenda majirani zetu ambao wamekuwa hapa kwa miongo kadhaa, wale ambao wameishi hapa kwa karne nyingi, kama vile sisi tunavyowapenda na kuwaheshimu marafiki zetu wa asili ambao walikuwa hapa kabla ya hayo.